Blogu ya kennytz
inayomilikiwa na Kenneth Paul ni blogu ya Kitanzania yenye dhumuni la kukuza
matumizi ya lugha ya Kiswahili. Katika kennytz, utapata kusoma masimulizi
mbalimbali yanayoandikwa na Kenneth Paul ambaye ni msomi mwenye upeo mkubwa wa
kuelewa lugha. Masimulizi ya Kenneth Paul utakayoyasoma katika kennytz yatakuwa
yakitumia lugha ya Kiswahili yenye usanifu mkubwa ili kupitia masimulizi hayo,
uweze kupata picha yaani ufahamu juu ya matumizi sahihi ya lugha yetu ya
Kiswahili. Hata hivyo baadhi ya masimulizi yanaweza kuwa katika lugha ya
Kiingereza kwa ajili ya kutoa burudani kwa wale wapenzi wasiofahamu lugha ya
Kiswahili.
Pia katika
kennytz, kuna kipengele cha kucheka na kuchekesha ambapo kurasa zake zinalenga
maswala ya vichekesho. Kenneth Paul ni kati ya watu wenye uwezo mkubwa wa
kuchekesha na kupitia utaalamu wa Kenneth Paul wa kudadisi na kupembua mambo,
amejaribu kutafuta mambo mbali mbali yanayohusiana na swala la kucheka na
kuchekesha watu.
Kennytz itakupa
mafunzo ya lugha ya maneno, yaani kusikiliza kwa umakini maneno watumiayo watu
ili kuelewa dhamira ya mazungumzo. Vile vile katika kujifunza huko, utaweza
kujua maneno sahihi ya kutumia ili kuweza kufanikisha malengo ya kauli zako,
kama ni kuchekesha, kuuliza swali, kutoa taarifa, kuomba msamaha, kushawishi na
mengine mengi.
Kennytz pia
inajaribu kuelezea mafunzo mbali mbali kutoka katika filamu ndani na nje ya
Tanzania. Kenneth Paul ni mpenzi wa filamu na amekuwa akijifunza mengi kuhusu
maisha kupitia filamu. Lakini Kenneth Paul amekuwa akishangazwa na namna watu
wanavyochukulia kwamba filamu zipo tu kwa ajili yta kuburudisha na si
kufundisha. Hivyo Kenneth Paul anafichua mafunzo mbali mbali kutoka katika
filamu kupitia kennytz ambayo yatasaidia watu katika maisha.
Karibu na tembelea
kennytz ya Kenneth Paul mara kwa mara kwa ajili ya burudani na mafunzo.
No comments:
Post a Comment