Kabla ya kukicha,
majira ya saa kumi na moja na nusu alfajiri, baba Kayumbas anaamka na kuondoka
kwenda kazini. Mama Kayumbas na akina Kayumbas wanaamka saa kumi na mbili na
kufanya shughuli zao. Ndiyo ratiba yao ya siku zote.
Miezi kadhaa inapita
huku maisha yakienda vizuri hata baba Kayumbas kuweza kuwanunulia wanawe
runinga mwezi mmoja tu tangu akubaliane na mkewe swala hilo na sasa ameanza kuweka
akiba kwa ajili ya kununua kiwanja hapa
Dar na baadaye kuweza kujenga nyumba ndogo kwa ajili ya familia yake.
Miezi inakwenda huku
kila leo ikiwa kama jana na kesho kutegemewa kuwa kama leo hadi unapofika mwezi
wa kwanza ambapo watoto wanapanda darasa moja mbele na Mjanja kuanza chekechea.
[Endelea kufuatilia simulizi hili litokanalo na matukio ya kweli...]
No comments:
Post a Comment