Habari tena wasomaji na watembeleaji wa blogu hii...
Kipengele hiki kinalenga kukupatia kicheko cha kudumu. Kipengele hiki hakidhamirii kuweka vichekesho mbalimbali kwa ajili ya watu kucheka na kuvitumia kuchekesha wengine. Hii ni kwa sababu ya uwepo wa vyanzo vingi vya vichekesho katika mitandao lakini blogu hii inaamini kwamba swala la kucheka au kuchekesha ni swala linalotegemea mengi na si tu mpangilio wa maneno ya kuchekesha. Ni malengo ya kipengele hiki kumpa mtu njia mbalimbali anazoweza kutumia ili kutoa vichekesho vya kipekee yaani vya kwake binafsi na si kukariri vichekesho vya watu wengine. Hata hivyo, ni mategemeo ya blogu kwamba katika kujifunza huko, utakuwa ukijichekea mwenyewe ukijua ya kuwa punde uelewapo njia moja, kuna wenzako wa kucheka nawe. Ndiyo, cheka na kuchekesha...
No comments:
Post a Comment